Features
January 25, 2022

Mbolea Za Yara Zimeleta Mapinduzi Ya Kilimo Kwa Wakulima Tanzania

Tutaendelea kujivunia kwa kusema “Kilimo bora huanza na matumizi ya virutubisho sahihi kwa mimea hivyo, Wakulima waliofanikiwa wametumia mbolea bora kutoka Yara. Karibu unufaike na chachu hii ya maaendeleo ya sekta ya kilimo.


Mbolea Za Yara Zimeleta Mapinduzi Ya Kilimo Kwa Wakulima Tanzania
Mbolea Za Yara Zimeleta Mapinduzi Ya Kilimo Kwa Wakulima Tanzania

Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita kampuni ya Yara imekuwa mdau muhimu katika maendeleo ya sekta ya kilimo jambo lililowanufaisha wakulima wadogo na kutoa mchango katika uchumi wa Taifa.

Yara ni kampuni inayojishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa mbolea. Yara ilianzishwa Oslo, Norway mwaka 1905 kwa lengo la kuondoa njaa duniani na kutunza mazingira.

Baada ya hapo ilienea katika nchi zaidi ya 160 kwenye mabara yote duniani. Yara ina ofisi kwenye nchi zaidi ya 50 na viwanda katika mabara yote.

Ili kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa na tija na kuwanufaisha wakulima na Taifa kwa ujumla, mwaka 2020 kampuni hiyo ilizindua mpango maalumu wa kusaidia sekta ya kilimo Tanzania.

Chini ya mpango huo, unaojulikana kama ‘Action Africa’, uzalishaji wa mazao ya mpunga na mahindi umeongezeka sambamba na kumhakikishia mkulima mdogo chakula na kuinua kipato cha familia kwa kuongeza uzalishaji.

Mpango huo unamsaidia mkulima kulima kilimo cha kisasa na bora kitakachomsaidia kujikwamua na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Pia lengo la mpango huu ni kukuza uzalishaji wa mahindi na mpunga na kuihakikishia nchi usalama wa chakula.

Katika mpango huo, mbolea tani 12,500 ziliitengwa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima masikini nchini. 

Mbali na hayo Yara ndiyo kampuni ya kwanza duniani kutengeneza mbolea za kilimo tangu mwaka 1905 na inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 160 duniani. Yara imesajiliwa na Shirika la Viwango Duniani (ISO) ili kuendana na viwango halisi. 

Mbolea za Yara zimegawanyika katika makundi makuu matano, hiyo yote ni kutokana na aina ya udongo na mazao maana pia kila zao lina uhitaji na biolojia tofauti. Makundi hayo ni;

YaraMila

YaraMila ni jamii ya mbolea zenye virutubisho vya msingi (NPK), vya kati (S, Mg, Ca) na vidogo (Zn, B, Mn) ili kuupa mmea lishe kamili na linganifu kwa uzaaji wa mazao mengi na bora.

Katika kuzingatia uhitaji wa virutubisho kwa kila zao kuna YaraMila CEREAL (23-10-5 NPK +3S +2MgO +0.3Zn) mahususi kwa ajili mazao ya nafaka kama vile (mahindi na mpunga),YaraMila WINNER(15-9-20 NPK +3.8S+1.8MgO+0.2 Zn+0.2 B+ 0.2Mn) kwa ajili ya mbogamboga, viazi mviringo na matunda kama parachichi, ndizi, pesheni na papai),YaraMila JAVA(22-6-12 NPK +3S +1MgO +2 CaO +0.2B+ 0.2Mn) kwa ajili ya kahawa, miwa na matunda),YaraMila TOBACCO(10-18-24 NPK +7S +3 CaO +0.5MgO +0.1B) kwa ajili ya zao la tumbaku), YaraMila UNIK (17-17-17 NPK) kwa ajili ya kupandia na kukuzia mazao mbalimbali na YaraMila OTESHA(13-24-12 NPK +Sulphur+magnesium + Zinc ni kwa ajili ya kupandia mazao yote.

Mbolea za Yaramila zinafanya vizuri katika udongo wa aina mbalimbali hata kwenye maeneo yenye udongo uliochachuka na yenye upungufu wa mvua.

YaraLiva

Kundi hili ni mbolea jamii ya Calcium Nitrate kama vile YaraLiva NITRABOR (15.4N+ 25.6 CaO +0.3B), YaraLiva CALCINITY (15.5 N+26.3 CaO). Mbolea hizi zina Calcium inayoyeyuka kwa haraka ili kukidhi uhitaji wa Calcium kwa mmea husika katika kuongeza ubora wa mazao, kuzuia kuoza kwa nyanya kwenye kitovu, kupasuka kwa matunda kama ndizi au parachichi kabla hayajakomaa, kuwa na mvuto sokoni, uhifadhi wa muda mrefu na uharibifu wakati wa usafirishaji.

YaraBela

Mbolea hizi ni jamii ya Ammonium Sulphate Nitrate zenye Nitrojen na Sulphur kama vile YaraBela SULFAN (24 N: 6S: 11 CaO ambayo ni kwa ajili ya kukuzia na kuzalishia mazao ya nafaka, viazi, nyanya, vitunguu, mbogamboga na matunda kama ndizi.

YaraVera

Mbolea za jamii ya Urea ambazo ni YaraVera AMIDAS (40N: 6S) yenye nitrojeni na sulphur na YaraVera AMIGRAN (46%N). Hizi ni mbolea za kukuzia mazao mbalimbali zikiwemo ya nafaka kama mahindi na mpunga.

MiCROP

Jamii ya mbolea za kupan­dia na kukuzia mazao ya nafaka inayotengenezwa hapa nchini (Fahari ya Mtanzania).

MiCROP (17:29:6 NPK +7 S +0.2 Zn) ni mbolea ya kupan­dia mazao ya nafaka kama vile mahindi, mpunga, shayiri na MiCROP Mbolea ya kuku­zia (46%N +0.2%Zn) ni mbolea ya kukuzia mazao ya nafaka kama vile mahindi, mpunga, shayiri.

YaraVita

Ni jamii ya mbolea za kunyunyizia kwenye majani kwa mazao yote hususani katika hatua za ukuaji na uzaaji. Mbolea hizi ni YaraVita CROP BOOST(44 (P2O5)+7.5(K20),6.6 MgO +4.6 Zn), YaraVita POWER BOOST(14 Zn+7 B +12 Mg +7 N), YaraVita TRACEL BZ (5%B, 5%Zn, 0.1%Cu, 0.1%Fe, o.1%Mn, 0.1%Mo, 5%N, 7.5% (P205), 5%(K20),5%Mg,5%S).

Ili kukidhi uhitaji ya virutubisho mbalimbali hususani vidogovidogo pia kuuwezesha mmea kupata virutubisho kipindi cha changamoto za hali ya hewa kama vile ukame au baridi.

 

Wakulima waliofanikiwa kwa kutumia mbolea za Yara wazungumza

Daniel Steven mkulima wa mahindi Kata ya Mwangata mkoani Iringa anasema amelima kwa muda mrefu kwa kutumia mbolea nyingine lakini mwaka 2017 alipata elimu kuhusu mbolea za Yara.

“Mwaka 2017 nilielimishwa kuhusu ubora wa mbolea za Yara na ndipo nilipozifahamu. Kutokana na ubora wa mbolea hizo nilipata manufaa makubwa katika kilimo changu kwani kipindi cha nyuma nilitumia mbolea ambazo hazikuniletea manufaa kama haya,” anasema Steven.

Anasema tangu ameanza kutumia mbolea za Yara mavuno yameongezeka kwani kipindi cha nyuma alikuwa anapata gunia 11 hadi 12 kwa ekari lakini baada ya kuanza kutumia mbolea za Yara mavuno yameongezeka na sasa anapata mpaka gunia 34 kwa ekari moja.

“Mavuno haya yameongezeka kutokana na kutumia mbolea za Yara aina ya YaraMila OTESHA na YaraVera AMIDAS na kuniletea mafanikio makubwa ambapo sasa nina mpango wa kupanua shughuli zangu za kilimo kwa kutafuta mashamba mengine,” anasema Steven.

Ipiana Kayuni mkulima wa miwa kutoka Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro anasema Yara imemsaidia kuboresha kilimo chake.

“Hapo awali nilikuwa na shaba la ekari moja, baadaye nikapanda mpaka tano na sasa namiliki shamba la ekari nane. Kwa kawaida kwenye kilimo changu natumia mbolea za Yara kwa sasa kwani nazipenda na zinanipa manufaa makubwa,” anasema Kayuni.

Anasema huwa anaanza kutumia mbolea ya kupandia aina ya YaraMila OTESHA, baada ya kupanda hutumia ya kukuzia aina ya YaraVera AMIDAS ambazo anadai zimempa manufaa makubwa kwa kuboresha kilimo chake na kumuongezea mavuno.

“Mbolea za Yara zimenionyesha maajabu makubwa kwani haziharibu udongo na badala yake zimenisaidia katika kuongeza rutuba kwenye shamba langu,” anasema Kayuni.

Anasema kipindi cha nyuma alikuwa mkulima wa mbogamboga na sasa anamiliki shamba la miwa. Manufaa makubwa ameyapata kwani sasa amejenga nyumba, amenunua trekta, amepeleka watoto shule na amefungua kiwanda cha kukoboa mpunga, haya yote yametokana na kutumia mbolea za Yara.

Veronica Urio mkulima wa mpunga kutoka Dakawa, Mvomero Morogoro anasema katika ukulima wake alikuwa analima kilimo cha kawaida lakini kuanzia mwaka 2012-13 alipata mbolea za Yara na kufanikiwa kubadili kilimo chake kuwa cha manufaa zaidi.

“Mbolea ya kwanza niliyotumia ni YaraMila OTESHA ambayo natumia siku saba baada ya kupandikiza, kuanzia siku 14 hadi 21 natumia YaraVera AMIDAS pamoja na mbolea ya kunyunyizia kwenye majani aina ya YaraVita CROP BOOST na mbolea ya mwisho ni YaraLiva NITRABOR ambayo naitumia muda mfupi kabla ya mpunga kuchanua (mimba dume),”anasema Veronica.

Anasema mbolea za Yara zina virutubisho vingi ambavyo vinamsaidia kuvuna mpunga unaotoa mchele bora, mnene, mzito na usio na chenga jambo linalomtofautisha na wakulima wengine wasiotumia mbolea hizo.

Mkulima wa mahindi Elisante Mmanga kutoka Sumbawanga mkoani Rukwa anasema matumizi ya mbolea bora za Yara yamemletea manufaa makubwa katika kilimo chake tofauti na kipindi cha nyuma.

“Nilipopanda baada ya kuota nilitumia mbolea ya YaraMila CEREAL ambapo niliona mahindi yangu yana mwelekeo mzuri. Baada ya muda kupita nikatumia YaraVita CROP BOOST ambayo nilipuliza siku ya 14, wiki ya sita nilirudia kuweka YaraMila CEREAL jambo lililonisaidia kuvuna mahindi mengi na yaliyojaa vizuri,” anasema Mmanga.

Jonas Mwashamba mkulima wa mahindi kutoka Mbozi, Songwe anasema alitumia MiCROP mbolea ya kupandia na ilipofika wiki ya tatu alitumia YaraVita CROP BOOST na wiki ya tano alitumia MiCROP mbolea ya kukuzia ambazo zilimsaidia kupata mavuno mengi.

Tutaendelea kujivunia kwa kusema “Kilimo bora huanza na matumizi ya virutubisho sahihi kwa mimea hivyo, Wakulima waliofanikiwa wametumia mbolea bora kutoka Yara. Karibu unufaike na chachu hii ya maaendeleo ya sekta ya kilimo”.